Rodri
Rodri katika Kombe la Dunia la FIFA 2026 | |||
| Taarifa binafsi | |||
|---|---|---|---|
| Jina kamili | Rodrigo Hernández Cascante | ||
| Tarehe ya kuzaliwa | 22 Juni 1996 | ||
| Mahali pa kuzaliwa | Madrid, Hispania | ||
| Kimo | 1.91 m (6 ft 3 in) | ||
| Nafasi anayocheza | Kiungo ulinzi (CDM) | ||
| Taarifa za klabu | |||
| Klabu ya sasa | Barcelona | ||
| Namba | 16 | ||
| Kazi katika klabu | |||
| Miaka | Timu | Mechi† | (Goli)† |
| 2015–2016 | Villarreal B | 42 | (2) |
| 2015–2018 | Villarreal | 63 | (1) |
| 2018–2019 | Atlético Madrid | 34 | (3) |
| 2019–2026 | Manchester City | 196 | (23) |
| 2026– | Barcelona | 0 | (0) |
| Timu ya Taifa ‡ | |||
| 2012 | Hispania U16 | 2 | (0) |
| 2014–2015 | Hispania U19 | 8 | (0) |
| 2017–2018 | Hispania U21 | 6 | (1) |
| 2018– | Hispania | 78 | (5) |
| * Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 18 Agosti 2026. † Appearances (Goals). | |||
Rodrigo Hernández Cascante (alizaliwa 22 Juni 1996), anajulikana zaidi kama Rodri au Rodrigo, ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nchini Hispania anayecheza kama kiungo ulinzi katika klabu ya Barcelona na Timu ya taifa ya Hispania.
Anachukuliwa kwa kiasi kikubwa kuwa mmoja wa viungo bora zaidi duniani kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi, utulivu uwanjani na umbo lake la kimwili. Rodri ni mmoja wa wachezaji wachache waliowahi kutwaa mataji ya Kombe la Dunia la FIFA, Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) na tuzo ya Ballon d'Or. Alipata tuzo ya Ballon d'Or mwaka 2024, na kuwa mchezaji wa pili wa Hispania[1] na mchezaji wa kwanza wa Manchester City kutwaa tuzo hiyo.[2]
Maisha ya awali na klabu
Villarreal
Rodrigo Hernández Cascante[3] alizaliwa 22 Juni 1996[4] mjini Madrid.[5] Alijiunga na mfumo wa vijana wa Atlético Madrid mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 11 kutoka CF Rayo Majadahonda.[6] Mwaka 2013, aliachwa na klabu hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa "ukosefu wa nguvu za kimwili", na baadaye alisaini mkataba na Villarreal.[7]
Mnamo 7 Februari 2015, Rodri alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya akiba ya Villarreal B.[8] Alianza kucheza rasmi katika timu ya wakubwa mnamo 17 Desemba 2015 kwenye ushindi wa mabao 2–0 dhidi ya SD Huesca katika mchezo wa Copa del Rey.[9] Mechi yake ya kwanza katika ligi kuu ya La Liga ilikuwa 17 Aprili 2016 akiingia kama mchezaji wa akiba kuchukua nafasi ya Denis Suárez dhidi ya Rayo Vallecano.[10]
Atlético Madrid
Mnamo 24 Mei 2018, Rodri alirejea Atlético Madrid baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano na Villarreal kwa ada iliyokadiriwa kuwa euro milioni 20.[11] Alisaini mkataba wa miaka mitano na alicheza mechi yake ya kwanza tarehe 15 Agosti kwenye UEFA Super Cup ya mwaka 2018 mjini Tallinn, ambapo Atlético ilishinda 4–2 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Real Madrid. Alishinda pia tuzo yake ya kwanza ndani ya klabu hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora katika safu ya kiungo.[12]
Manchester City
Mnamo 3 Julai 2019, Manchester City ililipa pauni milioni 62.6 kuvunja mkataba wake na Atlético Madrid, ada iliyokuwa rekodi ya usajili kwa klabu hiyo kwa wakati huo.[13]
Akiwa na Manchester City, Rodri alikuwa nguzo kuu katika kikosi cha kocha Pep Guardiola. Alisaidia klabu hiyo kutwaa mataji manne mfululizo ya Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) na kukamilisha rekodi ya kutwaa mataji matatu makubwa kwa msimu mmoja (treble) katika msimu wa 2022–23. Mnamo 10 Juni 2023, alifunga bao pekee la ushindi katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) dhidi ya Inter Milan,[14] na kuipatia Manchester City taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa, ambapo alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Msimu wa mashindano hayo.[15]
FC Barcelona
Mnamo 18 Agosti 2026, Rodri alikamilisha uhamisho wake wa kurejea nchini Hispania baada ya kusajiliwa na klabu ya Barcelona kwa mkataba wa miaka minne.[16] Uhamisho huo uligharimu kiasi cha pauni milioni 65.4 (euro milioni 76.5).[17] Katika kikosi cha Barcelona, alikabidhiwa jezi namba 16, akichukua nafasi ya kiungo ulinzi kufuatia mabadiliko ya kikosi cha timu hiyo kwa msimu wa 2026–27.
Timu ya taifa
Baada ya kuwakilisha Hispania katika ngazi za vijana, Rodri alichaguliwa kwenye timu ya wakubwa mnamo 16 Machi 2018.[18] Alicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani tarehe 11 Septemba kwenye ushindi wa 6–0 dhidi ya Kroatia katika mashindano ya UEFA Nations League.[19]
Alikuwa muhimili mkubwa katika kuifanya timu ya taifa ya Hispania kutwaa mataji ya UEFA Nations League (2023), UEFA Euro 2024, pamoja na Kombe la Dunia la FIFA 2026. Katika mafanikio hayo, Rodri alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano kwenye Euro 2024 na pia kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Tuzo na mafanikio

Atlético Madrid
- UEFA Super Cup: 2018
Manchester City
- Ligi Kuu ya Uingereza (EPL): 2020–21, 2021–22, 2022–23, 2023–24
- FA Cup: 2022–23
- EFL Cup: 2019–20, 2020–21
- Ngao ya jamii: 2019
- Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA): 2022–23
- UEFA Super Cup: 2023
- Kombe la Dunia la Klabu la FIFA: 2023
Hispania U19
- UEFA Euro U-19: 2015
Hispania
- UEFA Euro 2024
- UEFA Nations League: 2022–23
- Kombe la Dnunia la FIFA: 2026
Binafsi
- Mshindi wa Ballon d'Or: 2024[20]
- Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia la FIFA (Mpira wa Dhahabu): 2026[21]
- Mchezaji Bora wa Mashindano ya Euro (UEFA): 2024[22]
- Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA): 2022–23[23]
- Mchezaji Bora wa Mashindano ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya (UEFA): 2023[24]
- Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia la Klabu la FIFA (Mpira wa Dhahabu): 2023[25]
Marejeo
- ↑ "Ballon d'Or 2024: Manchester City and Spain midfielder Rodri wins first award". BBC Sport. 28 Oktoba 2024. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rodrigo becomes first City player to win Ballon d'Or". OneFootball. 30 Oktoba 2024. Iliwekwa mnamo 30 Oktoba 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Acta del Partido celebrado el 18 de mayo de 2019, en Valencia" (kwa Kihispania). Royal Spanish Football Federation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 17 Juni 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rodri". ESPN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 19 Februari 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rodri: Summary". Soccerway. Perform Group. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 6 Aprili 2024.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Fútbol: el nuevo fichaje "Rodri" (At. Madrid) y Lucas jugaron juntos en Majadahonda" (kwa Kihispania). Majadahonda Magazin. 22 Desemba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "El Busquets que se le escapó al Atlético VS. el nuevo 'kaiser' rojiblanco". Mundo Deportivo (kwa Kihispania). Barcelona. 16 Julai 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Desemba 2015. Iliwekwa mnamo 18 Desemba 2015.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "1–3: Frenados" (kwa Kihispania). RCD Espanyol. 7 Februari 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Desemba 2015. Iliwekwa mnamo 18 Desemba 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Trigueros remonta al Huesca y certifica el pase sin presumir". Diario AS (kwa Kihispania). Madrid. 17 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Desemba 2015. Iliwekwa mnamo 18 Desemba 2015.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dos misiles de Guerra y Miku hunden al Submarino". Diario AS (kwa Kihispania). Madrid. 17 Aprili 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Juni 2018. Iliwekwa mnamo 3 Juni 2018.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Acuerdo con el Villarreal para el traspaso de Rodri" (kwa Kihispania). Atlético Madrid. 24 Mei 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Juni 2019. Iliwekwa mnamo 24 Mei 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rodri: Who is the Spain international and what will he bring to Man City?". BBC Sport (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2019-07-04. Iliwekwa mnamo 2026-07-21.
- ↑ "Rodri: Manchester City pay £62.6m release clause for Atletico Madrid's Spain midfielder". BBC Sport. 3 Julai 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 3 Julai 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Manchester City 1–0 Inter Milan". BBC Sport. 10 Juni 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rodri named 2022/23 UEFA Champions League Player of the Season". UEFA. 11 Juni 2023. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2023.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "FC Barcelona sign Rodrigo Hernández". www.fcbarcelona.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-08-18.
- ↑ "Rodri joins Barcelona from Man City in £65m deal". BBC Sport (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2026-08-18. Iliwekwa mnamo 2026-08-18.
- ↑ "Parejo, Marcos Alonso y Rodri, novedades en la lista de la selección española". El País (kwa Kihispania). Madrid. 18 Machi 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Aprili 2019. Iliwekwa mnamo 28 Machi 2018.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "España 6–0 Croacia: resultado, resumen y goles". AS. 23 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 20 Juni 2024.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Ballon d'Or 2024: Manchester City and Spain midfielder Rodri wins first award". BBC Sport. 28 Oktoba 2024. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Imber, Leon (2026-07-20), "Spain's Rodri wins World Cup Golden Ball as Pau Cubarsi, Unai Simon also collect awards", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2026-08-11
- ↑ UEFA.com. "Season 2024 | UEFA EURO 2024". UEFA.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-08-11.
- ↑ "Rodri named 2022/23 UEFA Champions League Player of the Season". UEFA. 11 Juni 2023. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2023.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ UEFA.com (2023-06-18). "Rodri named 2023 UEFA Nations League Player of the Finals | UEFA Nations League 2023". UEFA.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-08-11.
- ↑ www.fifa.com https://www.fifa.com/en/tournaments/mens/fifa-club-world-cup/saudi-arabia-2023/articles/award-winners-revealed-manchester-city-rodri-walker-arias. Iliwekwa mnamo 2026-08-11.
{{cite web}}: Missing or empty|title=(help)