Uhandisi wa kiraia

Uhandisi wa kiraia (kutoka king Civil Engineering) ni taaluma ya uhandisi ambayo inahusika na usanifu, ujenzi, na matengenezo ya mazingira halisi na mazingira yaliyojengwa kiasili, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, madaraja, mifereji ya maji, mabwawa, viwanja vya ndege, mifumo ya maji taka, mabomba, mihimili ya majengo na reli.[1][2]
Kwa kawaida uhandisi wa kiraia umegawanyika katika taaluma nyingine ndogondogo. Inachukuliwa kama taaluma ya pili kwa ukongwe baada ya uhandisi wa kijeshi.[3] Uhandisi wa kiraia unaweza kufanyika kwenye sekta ya umma kuanzia katika ngazi ya halmashauri hadi serikali kuu, na kwenye sekta ya umma kuanzia kampuni ndogo hadi kampuni za kimataifa za ujenzi.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Fani ya uhandisi wa kiraia hutumia kanuni za kisayansi kwa ajili ya kutatua matatizo katika jamii, na historia yake inahusishwa kwa karibu na maendeleo katika uelewa wa fizikia na hisabati.Kwa sababu uhandisi wa majengo ni taaluma pana, imesaidia kuchangia maarifa katika nyanja nyingine kama jiografia, jiolojia, udongo, haidrolojia, sayansi ya mazingira, mitambo, na usimamizi wa mradi.[4]
Katika historia ya kale na ya zama za kati, mara nyingi usanifu majengo na ujenzi ulikuwa ukifanywa na mafundi, kama vile waashi na maseremala, ambao walipanda cheo na kuwa mafundi wakuu. Maarifa yalibaki katika vyama vya mafundi na mara chache sana maarifa hayo hayakubadilika. Miundo, barabara na miundombinu iliyokuwepo ilikuwa ya kurudia rudia.[5]
Mojawapo ya mifano ya awali ya matumizi ya mbinu za kisayansi na hisabati katika uhandisi wa kiraia ni kazi ya Archimedes katika karne ya 3 KK, ikiwemo Kanuni ya Archimedes, ambayo ndiyo msingi wa uelewa wetu kuhusu ueleaji, na skrubu ya Archimedes. Brahmagupta, mwanahisabati wa Uhindi, alitumia hesabu katika karne ya 7 BK, katika nambari za Kihindu-Kiarabu, kwa ajili ya hesabu za uchimbaji.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "History and Heritage of Civil Engineering". American Society of Civil Engineers. Archived from the original on 16 February 2007. Retrieved 8 August 2007.
- ↑ "What is Civil Engineering". Institution of Civil Engineers. 14 January 2022. Retrieved 15 May 2017.
- ↑ "What is Civil Engineering?". Canadian Society for Civil Engineering. Archived from the original on 12 August 2007. Retrieved 8 August 2007.
- ↑ Baveystock, Nick (8 August 2013). "So what does a civil engineer do, exactly?". The Guardian. Retrieved 11 September 2020.
- ↑ Saouma, Victor E. "Lecture Notes in Structural Engineering" (PDF). University of Colorado. Archived from the original (PDF) on 19 April 2011. Retrieved 2 November 2007.
- ↑ Colebrook, Henry Thomas (1817). Algebra: with Arithmetic and mensuration. London.