Nenda kwa yaliyomo

Abdelaziz Bouteflika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abdelaziz Bouteflika

Abdelaziz Bouteflika mwaka 2008
Amezaliwa 2 Machi 1937
Amekufa 17 Septemba 2021
Nchi Algeria
Majina mengine Abdelaziz Bouteflika
Kazi yake Mwanasiasa
Cheo Rais wa Algeria

Abdelaziz Bouteflika (2 Machi 1937 – 17 Septemba 2021) alikuwa mwanasiasa wa Algeria ambaye alikuwa Rais wa Algeria kuanzia 27 Aprili 1999 hadi 2 Aprili 2019, kwa karibu miaka 20: ndiye rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Algeria.

Bouteflika alizaliwa Oujda, Moroko, mwaka 1937. Baada ya Algeria kupata uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1962, alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya Algeria, ikiwa ni pamoja na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria.

Mwaka 1999, Bouteflika alichaguliwa kuwa rais wa Algeria. Alihudumu katika kipindi cha miaka minne mfululizo, hadi alipojiuzulu tarehe 2 Aprili 2019 kufuatia maandamano makubwa nchini Algeria.

Alifariki tarehe 17 Septemba 2021 akiwa na umri wa miaka 84.